Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Omar Said Shaaban amewaonya baadhi ya Wafanya Biashara Kisiwani Pemba wanaendelea kuwauzia Wananchi Bidhaa za Vyakula ikiwemo Sukari kinyume na Bei elekezi ilowekwa na Serikali.
Waziri Omar ametoa Kauli hiyo wakati akizungumza na Wafanya Biashara Masheha na Watendaji wa Wizara hiyo katika hafla ya ufunguzi wa Kituo cha utoa wa huduma ya usajili wa Biashara na Mali BPRA Mjini Chake Chake.
Amesema licha ya Serikali kutoa bei elekezi ya bidhaa ya Sukari lakini kuna baadhi ya Wafanya Biashara wamekuwa wakikiuka sheria.
Aidha Waziri Shaabani ameipongeza bpra kwa kuweza kuweka Kituo kidogo katika Mkoa wa Kusini Pemba Kituo ambacho kitaweza kurahisisha utoaji wa huduma ya usajili wa Bishasha na matukio kwa Wananchi wa Mkoa huo.
Kwa upande wake Mrajisi wa BPRA Pemba Mohammed ali maalim amesema pamoja na mafanikio yaliopatika ndani ya Taasisi hiyo lakni changmoto kadhaa ikiwemo uhaba wa Wafanya kazi.