MHANDISI ZENA AKEMEA TABIA YA KUWAFUNGIA NDANI WATOTO WENYE ULEMAVU

Iftaari Lulu Foundation

      Serikali imesema hairidhiswhi na tabia ya baadhi ya Wazazi ya kuwafungia ndani Watoto wenye ulemavu wa akili kwani kunawakosesha haki zao za msingi.

     Rai hiyo ameitoa mara baada ya Iftar iliyoandaliwa na Taasisi ya Lulu Foundation huko Ukumbi wa Shekh Idrissa Abdul Wakil Kikwajuni Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Mhandisi Zena Ahmed Said amesema hatua hiyo inasababisha kuikosesha Serikali Takwimu sahihi kwa Watoto hao kwa wanakosa haki zao wanazostahili ikiwemo Elimu afya pamoja na uangalizi mzuri wa Jamii.

     Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Lulu Foundation Lulu Abdalla Omar amesema mkusanyiko huo ni kuimarisha umoja, upendo na ushirikiano baina ya Jamii na Watoto hao ili kutoa elimu ya malezi kwa wazazi ili kuwawezesha Watoto hao kupata haki zao zote za Msingi.

    Prof Mohammed Hafidh Khalfan Mshauri na Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Lulu  ameipongeza Taasisi hiyo kwa juhudi wanazozifanya za kuwa karibu na Watoto hao na kuitaka Jamii kuunga mkono juhudi hizo.

    Taasisi ya Lulu foundation kabla ya Iftari hiyo kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali wamefanikiwa kuzifikia Familia zenye Watoto wenye  Ulemavu wa Akili 200 kwa kutoa misaada ya Chakula katika Maeneo mbalimbali ya Unguja ikiwemo Kiembesamaki ,Jangombe ,Mwera,Dole,Mahonda na Matemwe.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.