WADAU ELIMU KUSHIRIKI KUPANGA MAENDELEO YA ELIMU

Wadau Wizara ya Elimu

     Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imewatka Wadau wa Elimu Nchini kushiriki kikamilifu katika kupanga Mipango ya Maendeleo ya Elimu na Program mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha Elimu inaleta maendeleo kwa Mtu Mmoja Mmoja, Jamii na Taifa kwa Ujumla.

    Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo, ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati Akifungua Mkutano wa Mwaka wa pamoja wa Tathimini wa Sekta ya Elimu kwa Mwaka 2023/24  kwa Niaba ya Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda

  Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Tamisemi, Dk .Charles Msonde amesema Serikali inajitahidi kuboresha mazingira pamoja na kutatua changamoto za Walimu Nchini.

   Awali, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. James Mdoe amesema kuwa  Mkutano huo Wadau kwa pamoja watajadili changamoto na mafanikio katika Sekta ya Elimu na  kuja na Mikakati ya kuboresha Sekta hiyo.

Tags
stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.