WANAFUNZI MPENDAE WATAKIWA KUSOMA KWA MALENGO

Mbunge Mpendae

    Mbunge wa  Jimbo la Mpendae Mhe.Taufiki Salum Turki amewakumbusha  Wanafunzi wa Skuli ya Mpendae kusoma kwa  malengo ili waje kuwa Viongozi wa baadae.

    Akizungumza katika  Hafla  kutoa Chakula na Projector kwa Wanafunzi wa Kidatu cha Sita wa Skuli ya Mpendae amesema  kuyatambua malengo yao kutamuwezesha Mwanafunzi kujitambua.   

     Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Mpendae  Chausiku Mwinyi Pandu amewashukuru Viongozi wa Jimbo kwa kuendelea kuwaunga Mkono  na kuahidi kufanya vizuri kwa kuongeza Idadi ya Ufaulu .

     Wakati huo huo Mbunge huyo alikabidhi Mipira ya Maji kwa Viongozi wa Shehia pamoja Mskitini wa Kilimani  ili kuondosha tatizo la upatikanaji wa huduma ya Maji Safi na Salama 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.