Serikali itaendelea kuweka Mazingira Rafiki na wezeshi ya kiuchumi ili kukuza sekta ya Fedha Nchini.
Katika uzinduzi wa Ripoti ya utafiti Finscope Tanzania 2023 kwa upande wa Zanzibar, uliofanywa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla kwa Niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi ametaja miongozni mwa mikakati hiyo ni kuunda sera zinazozingatia mahitaji ya Sekta ya fedha.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, fedha na Mipango Dkt. Saada Mkuya Salum amesema kuna umuhimu wa kusambaza matokeo ya utafiti huo kupitia njia sahihi ili kunafanyika maamuzi na kubuni bidhaa na huduma zinazopatikana kirahisi, kwa gharama nafuu.
Kaimu Mkurugenzi Mfuko wa kuendeleza Sekta ya fedha Tanzania Erick Masinde amesema Ripoti hiyo imekuwa na lengo la kuikuza Sekta ya fedha na kuimarisha upatikanaji wa huduma ili kuwa jumuishi na endelevu na hatimae kurahisisha shughuli za Kiuchumi.
Kupitia Ripoti hiyo itazisaidia Serikali kukuwa kiuchumi hivyo wameiomba Serikali ya Zanzibar kuitumia Ripoti hiyo kuwa kielelezo cha kukuwa kwa maendeleo endelevu Nchini.