MAJAALIWA AONGOZA WANANCHI MAPOKEZI YA NDEGE BOEING 737-9MAX

MAPOKEZI YA NDEGE

     Waziri Mkuu Kasim Majaliwa amewataka Wafanya kazi wa Shirika la Ndege Tanzania ATCL kufanyakazi kwa uzalendo pamoja na kufanya tafiti za miruko ya Ndege ya ATCL ili kuweza kuleta tija na kuepuka kubadili ratiba za mara kwa mara za safari za Ndege za Shirika hilo.

    Waziri Mkuu Majaliwa ametoa kauli hiyo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl.Julius Nyerere Jijini Dar es salaam wakati wa mapokezi ya Ndege mpya aina ya Boeing 737-9Max ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali

     Amesema Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali  katika kuiwezesha Sekta ya uchukuzi ili kuweza kuchangia katika Uchumi wa Nchi ikiwemo Sekta ya Anga na Barabara.

    Kwa upande wake Waziri wa Uchukuzi Prof Makame Mbarawa amesema Wizara hiyo itaendelea kuziwezesha Taasisi zilizo chini yake ili ziweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na weledi.

    Nae Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) Ndg. Ladslaus Matindi amesema ujio wa Ndege hiyo           utaiwezesha kuongea miruko Ndege kikanda na Kimataifa kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl.Julius Nyerere. 

    Ndege hiyo inakuwa Ndege ya 14 kununuliwa na Serikali tangu kuanza kwa mpango wa ufufuaji wa ATCL Mwaka 2016 inauweza wa kubeba Abira 181imetengenezwa Nchini Marekani na kuigharamu Serikali ya Tanzania Kiasi cha Shilingi.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.