SHILINGI BILIONI 190.6 ZATUMIKA KUBORESHA MIRADI RUKWA

wakandarasi Rukwa

    Zaidi ya Shilingi  Bilioni 190.6 zimetumika Kujenga na kuboresha miradi ya kimkakati  Mkoani Rukwa katika kipindi cha Miaka 3 ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassani

   Meneja wa  Wakala wa Barabara Tanazia (tTanroads) Mkoa Rukwa Mhandishi Mgeni Mwanga ameeleza kuwa Mkoa huo umekwisha patiwa kiasi cha Fedha zaidi ya Bilioni 190.6 ,Fedha ambao zinatumika katika Ujenzi wa miradi 4 ya kimkaktaki katika Mkoa huo ambayo ni Ujenzi wa Barabara kiwango cha lami kutoka Sumbawanga hadi Kasanga yenye kilomita 107 , Barabara ya kutoka Matai hadi Kasesya mpakani mwa Zambia na Tanzania Kilomita 25, Mradi wa Barabara Kiwango cha lami kutoka Ntendo Muze hadi KilyaMatundu Kilomita 179 na Mradi wa upanuzi na ukarabati wa Uwanja wa Ndege Sumbawanga.

     Wakitoa Shukrani za pongezi kwa Rais Dkt.Samia baadhi ya Watumiaji wa Barabara Mkoani Rukwa wameeleza kuwa kumekuwa na mabadiliko makubwa sana katika Miundombinu ya Barabara ambao unawawezesha  kufanya shughuli zao za uzalishaji kiuchumi kwa wakati.

    Mkoa wa Rukwa ni Mkoa ambao umepakana na Nchi jirani kama vile Congo na Zambia hivyo uimara wa miundombinu ya Barabara unalenga kukuza  uchumi wa Tanzania  Kimataifa zikiwa zinapitika mda wote ,uharibifu wa Miundombinu hiyo unatajwa kuwa kikwazo ambapo Wananchi wametakiwa kutunza Miundombinu hiyo ambayo Serikali imetumia mda mwingi na gharama kubwa katika kuikamilisha ili iweze kuleta tija.

 

Tags
stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.