Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar itaendelea kushirikiana na Mashirika mbali mbali ya Kimataifa, ili kuhakikisha inaongeza ufaulu wa Masomo ya Sayansi na kuondosha Zero katika Mitihani ya Taifa.
Akizungumza katika Hafla ya kupongeza Mradi wa kuongeza ubora wa Elimu wa Skuli za Sekondari Zanzibar na namna ulivyofanikiwa pamoja na kugawa Vyeti kwa Walimu Wakuu na wasimamizi waliofanya vizuri baada ya kupatiwa Mafunzo, huko Ukumbi wa Samail Chake Chake Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe.Lela Mohamed Mussa, amethibitisha kuwa Mradi huo umeanza kuleta mafanikio kwa Skuli za Sekondari Visiwani Zanzibar.
Mapema Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ndg.Khamis Abdulla Said, amewataka Walimu pamoja na Maafisa Elimu waliopatiwa Mafunzo hayo kuongeza bidii ya usimamizi na ufatiliaji kiwango cha ufaulu kwa Masomo ya Sayansi yazidi kuongezeka.
Awali Naibu Mkurugenzi mkaazi KOICA Tanzania Mis. Jien Seong na Mkurugenzi Mkuu Good Neibours Soni jJung , wamesema ulipoanza mradi na sasa kuna mafanikio ya wazi ambayo yanaonekana.