Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo imewahimiza Wananchi kuendelea kuthamini juhudi za Serikali za kutunza Misitu kwa kuhakikisha Misitu inalindwa kwa maslahi yao na Taifa.
Akizungumza katika Hafla ya Upandaji wa Mikoko katika Maeneo yaliyoathirika ndani ya Msiti wa Jozani na kuwashirikisha Wananchi katika Kijiji cha Charawe, Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Shamata Shame Khamis amesema ni yema Jamii ikawa Mstari wa mbele kupinga hujuma dhidi ya Misitu ikiwa ni pamoja na kufuata taratibu na miongozo iliyowekwa.
Wananchi waliojitokeza wamewaomba Wananchi wa Maeneo yanayozunguka Misitu wa Jozani kuacha Tabia ya kukata Miti huku wakiomba Serikali kuendelea kuimarisha maslahi yanayotokana na fidia kwa ajili ya vipando vinavyoharibiwa katika Maeneo ya Msitu huo.
Wakati huo huo Waziri Shamata amezindua mradi wa mnara wa kuendeleza utalii wa kimaumbile katika Msitu wa Jozani Shehia ya Pete.
Siku ya Misitu Duniani huathimishwa kila ifikapo Tarehe 21/03 ya Kila Mwaka ambapo kauli mbili ya Mwaka huu Misitu na ubunifu ni suluhisho jipya kwa Dunia bora.