Kamati ya kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi imeihimiza Kamisheni ya kuakbiliana na Maafa Nchini kuendelea kuweka Mikakati Madhubuti katika kujiandaa na kukabiliana na maafa pindi yanapotokea ili kupunguza vihatarishi vya maafa Nchini.
Wajumbe wa Kamati hiyo Chini ya Mwenyekiti wake Mhe Machano Othman Said wametoa ushauri huo wakati wakipokea Taarifa ya Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2024 katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi wete Pemba.
Wameikumbhusha Kamisheni ya kukabiliana na Maafa umuhimu wa kujiandaa na kukabiliana na Maafa kwa kuzingatia Madhara yanayotokea pamoja na kufahamu Wajibu wa kila mmoja katika Eneo la kazi kuendelea kuchukua hatua stahiki endapo Maafa yanapotokea ili kuokoa Maisha na Mali za Jamii kutokana na Matukio hayo.
Nao Viongozi wa Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wakiwasilisha Taarifa ya utekelezaji wa Wizara hiyo wameihakikishia Kamati KWAMBA Wizara inaendelea kujipanga katika kufanyia kazi maelekezo yaliyotolewa na Kamati hiyo kwa kuzingatia umuhimu wa tahadhari za mapema ili kuendelea kuwa na nguvu ya pamoja katika kukabiliana na Maafa Nchini.