Viwanda vya kusindika Samaki vyafungwa kutokana na kukosa malighafi licha ya Mkoa wa Mara kuwa na asilimia 36 ya Ziwa Victoria jambo ambalo limepekea Mkoa huu kukosa Viwanda vikubwa .
Awali akisoma Taarifa ya hali ya Viwanda katika Mkoa wa Mara katika Baraza la Biashara Mkoa Afisa Biashara Mkoa Gambaless Timotheo amesema kukosekana kwa Samaki kumepleka kufungwa kwa Viwanda Vinne ambavyo vilikuwa vikisindika Samaki hao.
Wakichangia hoja ya ukosefu wa Samaki baadhi ya Wafanyabiashara wamesema Uvuvi Haramu ndio chanzo cha kukosekana Samaki ndani ya Ziwa na kuwatupia lawama Wavuvi wa Dagaa ambao hutumia Taa ambazo si rafiki kwa Samaki pamoja na matumizi ya Sumu na vilipuzi.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Mara amewataka Wanamara kubadilika kifikra kwa kuacha Uvuvi haramu na kufanya kazi ambapo amesema kama uvuvi haramu utaendela hakuna Viwanda vitakavyoweza kufanya kazi kama malighafi hazipo.