HALMASHAURI WATAKIWA KUTUMIA MAPATO YAO KUAJIRI WATUMISHI

ZIARA YA KUANGALIA JENGO LA MAMA NA MTOTO

    Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema ili kupunguza tatizo la uhaba wa Watumishi wa Sekta ya Afya linalozikabili baadhi ya Wilaya amezielekeza Halmashauri za Wilaya na Hospitali Nchini kutumia mapato yao ya ndani kuajiri Watumishi wa Kada hiyo kwa Mikataba.

    Waziri Ummy ameyasema hayo Jijini Mwanza wakati wa Ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na masuala ya Ukimwi ilipotembelea Mradi wa Jengo la Mama na Mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure.

     Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Dk. Bahati Msaky akitoa Taarifa ya uendeshaji wa huduma za Afya amesema Hospitali hiyo ina uwezo wa kulaza Wagonjwa 400 kwa wakati Mmoja.

     Mwenyekiti wa Kamati hiyo Stanslaus Nyongo ameipongeza Serikali kwa kuendelea kuimarisha Miundombinu ya Sekta ya Afya ikiwemo ununuzi wa vifaa tiba na mafunzo kwa Madaktari Bingwa Bobezi.

     Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Amina Makilagi amesema tangu kutokea kwa Mlipuko wa Ugonjwa wa Kipindupindu katika Wilaya Saba za Mkoa huo Jumla ya Visa 600 vya Ugonjwa huo vimeripotiwa kutokea Mkoani humo hadi kufikia Machi 12 Mwaka huu.

     Kamati ya Kudumu ya Bbunge ya Afya na masuala ya Ukimwi ikiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa huo Sekou Toure imetembelea Wodi ya Watoto wenye Vichwa vikubwa na Mgongo wazi, Wodi ya Wagonjwa wanaosumbuliwa na Vidonda vya Tumbo pamoja na Mradi wa Jengo la Mama na Mtoto ambalo limegharimu zaidi ya Shilingi Biloni 13.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.