Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan amekitaka Chama cha Wanawake Sekta ya Fedha TAWIFA, kuzingata miongozo ya Chama hicho waliojiwekea na kuzingatia Demokrasia, pamoja na kulipa kipaumbele suala la kumuwezesha Mwanamke kiuchumi ili kumkomboa kimaisha.
Rais Samia ameyasema hayo katika Uzinduzi wa Taasisi hiyo Kizimkazi, na kusema kuwa Wakati umefika wa kuhakikisha Mikakati ya kumkomboa Mwanamke katika kumuwezesha kiuchumi kielimu na maamuzi iwe kwa vitendo, na kujipanga kuweza kuwafikia wote.
Aidha amehimiza mshikamano katika utekelezaji wa majukumu yao kusaidiana maarifa na kuwataka kuondokana na sababu zitakazorejesha nyuma malengo yao.
Rais wa Chama cha Wanawake Sekta ya Fedha TAWIFA, Fikky Ntomola ameelezea baadhi ya matatizo yanayowakabili Wanawake wengi ni uelewa mdogo wa matumizi na usimamizi wa fedha, hivyo Taasisi hiyo ina mipango maalum ya kutoa elimu katika Sekta ya Fedha Afya na Uchumi
Naibu Kamishna Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania TIRA Ndg. Khadija Issa Said amesema Mamlaka itaendelea kusimamia Wanawake katika harakati zao za maendeleo hasa katika masuala ya umuhimu wa Bima.
Kongamano hilo la Siku moja limeandaliwa na TIRA, MIF na TAWIFA .