Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Mhandisi Zena Ahmed Said amesema Serikali itaendelea kushirikiana na Taasisi Binafsi katika kujenga Uchumi imara pamoja na kuwachukulia hatua wanaohusika na Ubadhirifu, Rushwa na Ufisadi.
Akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa kupambana na Rushuwa na Ufisadi kwa Makatibu na Naibu Makatibu Wakuu wa Taasisi Binafsi na za Umma juu ya masuali ya ubadhirifu na Rushwa ambapo amesema uchumi imara hujengwa kwa mtazamo na Vitendo vyema visivyo kuwa na Rushwa.
Amesema serikali inatambua mchango mkubwa unatolewa na Taasisi Binafsi katika kupambana na rushwa na ufisadi kama ni sehemu muhimu ya mapambano hayo.
Rais wa Taasisi ya Wataalamu dhidi ya Rushwa Bwana Ali Mbarouk
Amesema ili kutekeleza mpango Mkakati ni muhimu kushirikianana na Tasisisi Binafsi kwa kutoa Elimu na kuzalisha Wataalamu kwa ajili ya kujenga Uchumi imara nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya kuzuia Rushuwa na uhujumu Uchumi ZAECA Nd Ali Abdala Ali amesema kuwepo kwa Tasisi hiyo kutasaidia sana katika kuchukua hatua mapema na kupata Taarifa za rushuwa na uhujumu Uchumi.
Mkutano huo wa Siku Tatu umeandaliwa na Taasisi ya Wataalamu ya Rushwa na kupambana na ufisadi kutoka Dar Es Salam na ZAECA ambapo mada mbali mbali zimejadiliwa ikiwemo wajibu wa Viongozi wa umma katika kupambana na Ubadhirifu