SERIKALI ITAENDELEA KUWAWEZESHA WATANZANIA KUTUMIA NISHATI

WAZIRI MKUU TANZANIA

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema ataendelea kuwawezesha Watanzania kutumia Nishati safi ya kupikia ili ifikapo Mwaka 2030 zaidi ya asilimia 88  wawe wanatumia Nishati safi ya kupikia.

Ameyasema hayo  alipozungumza kwa njia ya Simu na Wanawake waliojitokeza katika Kongamano la kumpongeza kwa kuwa kinara wa Nishati safi ya Kupikia, Mazingira na Afya ya Mama na Mtoto yaliyofanyika katika Ukimbi wa Diamond Jubelee Dar Es Salaam, ambapo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alikuwa Mgeni Rasmi.

Kwa upande wake, Mheshimiwa Majaliwa ametoa Wito kwa Watanzania kumuunga Mkono Mheshimiwa Rais Dkt. Samia ili aweze kutimiza maono yake ya kuimarisha matumizi ya nishati safi ya kupikia, utunzaji wa mazingira pamoja na uimarishaji wa afya ya Mama na Mtoto kwa tija na ufanisi mkubwa. 

Kwa upande, wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo amesema Rais Dkt. Samia  anastahili kuitwa "Championi" wa Nishati safi ya kupikia na Mazingira kutokana na Jitihada kubwa alizozifanya kwa kutengeneza fursa za Watanzania kutumia nishati hiyo ikiwa ni pamoja na kusisitiza masuala ya utunzaji wa Mazingira.

Naye, Waziri wa maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi maalum Dkt. Doroth Gwajima amesema Rais Dkt. Samia ameendelea kuonesha Uongozi unaojali masuala ya Jinsia na Makundi maalum, kwa kuanzisha Wizara maalum pia kuwekeza katika Miundombinu ya Elimu kwa Watoto Wakike sambamba na kuwezesha mifumo rafiki kwa Wanawake.

Katika Mkutano huo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliendesha harambee ambayo ilifanikisha kupatikana kwa Shilingi Milioni 120 kwa ajili ya kumuwezesha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuchukua Fomu ya kugombea nafasi ya Urais katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.