DKT.BITEKO AWAONYA WATUMISHI KUACHA USUMBUFU KWA WAWEKEZAJI

Dkt.Biteko Dodoma

    Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe.Dkt.Doto Biteko,amewaonya Watendaji na Watumishi wa Umma wanaoendekeza Vitendo vya Urasimu na kuleta usumbufu kwa Wawekezaji wanaotaka kuwekezaji hapa Nchini.

    Dkt.Biteko ametoa maagizo hayo Jijini Dodoma wakati akizindua Rafiki Dodoma Hotel ambapo amesema kuwa Serikali inafanya kazi kubwa kuvuta Wawekezaji lakini kuna baadhi ya Watendaji wanakwamisha.

    Kwa upande wake Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda,amewataka Wawekezaji kuendelea kutumia vyema nia njema Serikali ya kuthamini Sekta Binafsi.

    Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Rafiki Dodoma Hotel Bw. fladmiry Mallya,amesema Uwekezaji huo ni katika kuunga Mkono juhudi za Serikali hasa kwenye Utalii.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.