Waandishi wa Habari Nchini wametakiwa kuandika Habari zinazohusu vitendo vya udhalilishaji na ukatili wa Kijinsia kwa Wanawake na Watoto, ambavyo vimekuwa na athari katika Jamii.
Akikabidhi Tunzo za umahiri wa Uandishi wa Habari za Takwimu za Vitendo hivyo, katika Skuli ya Shaa Mombasa, Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar, Ndg.Salum Kassim Ali, amesema Uandishi huo uzingatie vigezo ili kuweza kuleta mabadiliko dhidi ya vitendo hivyo.
Amesema kuwa, Takwimu zinaonesha kuongezeka kwa idadi ya vitendo vya udhalilishaji, hivyo Waandishi wa Habari wanawajibu kuendelea kuandika Habari ambazo zitangia kuinusuru Jamii na tatizo hilo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi Uchumi na Uwekezaji Ndg .Mariyam Juma Abdallah, amesema Wanawake Wengi hushindwa kugombea nafasi za uongozi kutokana na kutokua na kipato cha kutosha, na kuwataka kutumia fursa ya mikopo kwa Wajasiri amali.
Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania TAMWA Zanzibar Dkt. Mzuri Issa, amesema Tunzo hizo ni kushajihisha Waandishi wengi zaidi kuandika habari za Wanawake na Uongozi ili kuipa Jamii uwelewa na kuondosha vitendo hivyo.