Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeweka Bei elekezi kwa bidhaa ya Sukari ili kuwapa Wananchi unafuu wa maisha hasa katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan .
Akizungumza na vyombo vya Habari Waziri wa Biashara Maendeleo ya Viwanda Mhe Omar Said Shaaban amesema hatua hiyo itawasaidia Wananchi kwa kuwapunguzia kodi ya ushuru ili na wawe waweke bei ya bidhaa ya Sukari iweze kuwa chini ili kila mmoja aweze kuimudu kwa bei ya unafuu.
Ametoa Wito kwa Wafanya Biashara kujiepusha na vitendo vya Magendo ambapo atakaebainika hatua kazi zitachukuliwa dhidi yake.
Bei ya Sukari kwa upande wa Unguja itakuwa ni Shilingi Elfu 2 na Mia 650 na kwa upande wa Pemba ni elfu 2 na Mia 7.
hot
standard