Mhe.Wanu amesema hayo katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kwa Wanawake wa TRA kukabidhi msaada kwa Kituo cha Assalam Orphans Center.
Amesema kuwa kulea Yatima kunahitaji moyo na ni jambo kubwa kwa Mwenyezi Mungu. amesema kuwa Wanawake wa TRA wameweza kufanya jambo kubwa kwa kutoa na kuwatizama Watoto Yatima.
Mhe. Wanu amaahidi kushirikiana katika kuona Watoto hao wanapata huduma bora muda wote.
Meneja Rasilimali Watu TRA Zanzibar Zaina Salum akizungumzia Siku ya Wanawake amesema kuwa TRA itaendelea kuhamasisha kulipa kodi ili kuongeza kasi ya maendeleo.
Mkurugenzi Kituo cha kulelea Watoto Yatima cha Asalam Orphan Khadija Khamis Hamdan amesema Kituo kimeanza na Mtoto mmoja na sasa Watoto Yatima wameongezeka mara dufu ambapo ukuaji wa Kituo hicho unaenda sambamba na ongezeko la Watoto.
Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Zanzibar imetoa vitu mbali mbali ikiwema Chakula, Majiko ya kutumia Gesi na Fedha taslim pamoja na kula chakula cha Mchana pamoja.