Mtandao wa Polisi Wanawake Mkoa wa Arusha katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani wamefanya ibada maalumu kwa ajili ya kuwaombea Askari Polisi Wanandoa Waliofariki Dunia kwa ajali ya Gari Siku Mbili baada ya kufunga Ndoa.
Akiongea mara baada ya Ibada hiyo iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Theresia Jijini Arusha Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoani humo Mrakibu Msaidizi wa Polisi ASP Happiness Temu amesema Mtandao huo umekuwa na utaratibu wa kuyakumbuka makundi mbalimbali yenye uhitaji katika Jamii ambapo kwa Mwaka huu waliona ni vyema kuwakumbuka Askari Waliofariki kwa Ajali Disemba 20, 2022 Siku Mbili baada ya kufunga Ndoa
Baadhi ya Askari wa Mtaandao huo pamoja na kuwaombea Marehemu, pia wametumia ibada hiyo kumshukuru mungu kwa kuendelea kuwalinda katika utekelezaji wa majukumu yao.
Kwa upande wake Mrakibu wa Polisi SP Asia Matauka anaefanya kazi katika Mkoa wa Kilimanjaro amesema ni vyema kuungana na mtaandao huo kuwaombea Dua Marehemu.
Askari waliofariki na kufanyiwa Ibada leo ni Konstebo Noah Simfukwe na Agness Martin.