Kampuni ya Coca Cola imewataka Wajasiria Mali Wadogo kutumia fursa zinazojitokeza na kuwacha kuwa tegemezi katika Jamii .
Akizungumza katika Mafunzo ya kuwajengea uwezo Wajasiria mali Wadogo wadogo wa Chakula Afisa Uhusiano wa Umma Mawasiliano na uendelevu Kampuni ya Coca Cola Ndg.Maria Kimwaga amesema lengo la Mafunzo haya ni kuwaelimisha Wanawake katika maswala ya Biashara pamoja na kuhakikisha wanajiwezesha Kiuchumi .
Afisa Mikopo kutoka Wakala uwezeshaji Wananchi kiuchumi Ndg.Haji Khamis Ali ambae ni Mkufunzi wa Mafunzo hayo amewataka Wajasiria mali hao kuyatumia vyema Mafunzo waliopatiwa ili kujikwamua na hali ngumu ya Maisha na kutambua nafasi zao katika Jamii .
Wajasiria mali waliopata Mafunzo hayo wamesema wakabiliwa na matatizo mbali mbali ikiwemo kukosa nafasi maalumu za kufanyia kazi kupanda bei za bidhaa na kukosa mitaji jambo ambalo linawarejesha nyuma kiuchumi .