MTAALA MPYA WA ELIMU UTAMFANYA MWANAFUNZI KUBADILIKA

MHE LEILA MOHAMMED MUSSA

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Lela Mohamed Mussa amesema Wizara ya Elimu kupitia Taasisi ya Elimu inafanya mabadiliko ya Mtaala mpya ili kuhakikisha unamjenga Mwanafunzi kuendana na mabadiliko hayo.

Akizungumza katika zoezi la uzinduzi wa ugawaji wa Vitabu vya Mtaala mpya Waziri Lela amesema kupitia Vitabu hivyo vitamjenga Mwanafunzi na mabadiliko ya kusoma kwa Vitendo na kujifunza ipasavyo hivyo amewataka Walimu kuvitumia Vitabu hivyo kwa kuvifundisha ipasavyo.

Amesema atahakikisha anafanya Ziara za mara kwa mara kwa lengo la kuangali utumikaji wa Vitabu hivyo, ili Wanafunzi wanasoma kwa bidii na kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Aidha Mhe. Lela amewataka Wazazi na Walezi kuwasimamia Watoto kuhakikisha Vitabu hivyo wanavitumia na kuwaletea mabadiliko.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na mafunzo ya amali Dkt Mwanakhamis Adam Ameir amesema Kitabu ndio kinachomuongoza Mwalimu katika ufundishaji kwa Wanafunzi hivyo amewaomba Walimu hao kuvitumia Vitabu hivyo vya Mtaala mpya.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Elimu Abdallah Mohamed Mussa amesema Mtaala huo lazima uende na wakati uliopo hivyo Serikali zote mbili zinafanya juhudi kuhakikisha Sekta ya Elimu Nchini inakuwa na kutoa Wataalamu Wazuri wa baadae.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.