HALI YA UCHUMI ZANZIBAR KUKUA KWA ASILIMIA 7 NUKTA 2 KWA MWAKA 2024.

BARAZA LA WAWAKILISHI

Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango imesema mwelekeo wa hali ya uchumi kwa Mwaka  2024 unakadiriwa kukua kwa wastani wa asilimia 7 nukta 2.

Dk Mkuya mapitio akiwasilisha Taarifa ya mapitio na mwelekeo wa mpango wa Maendeleo na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025. Waziri wa Wizara hiyo Dkt Saada Mkuya Salum amesema ukuwaji huo wa uchumi utatokana na kuendelea kuongezeka kwa uingiaji wa Watalii kwa Asilimia 30 .

Amesema ukuaji huo wa uchumi pia utatokana na ongezeko la Mapato ya ndani yatokanayo na ongezeko la uwekezaji na utekelezaji wa mikakati ya ukusanyaji wa Mapato ya Serikali.

Akisoma Hotuba ya maoni ya kamati kuhusu mwelekeo wa mpango wa maendeleo na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2024/2025 Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti: Mh Mwanaasha Khamis Juma amesema ni vyema Serikali kuanza kufanya utafiti na tathmini ya kupata vyanzo vipya vya kuzalisha Umeme. Ikiwemo Umeme wa Jua na ,Umeme wa Joto la Ardhi.

Wakichangia hotuba hiyo Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wameishauri Serikali kuhakikisha Wakandarasi wanaopewa Miradi ya maendeleo ya Serikali kuwa wanatekeleza kwa umakini na uaminifu mkubwa.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.