Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe.Riziki Pembe Juma amekabidhi Nyumba Mama wa Mtoto mwenye ulemavu mchanganyiko Abdilah Kassim, ili kumuondelea shida ya makazi
Akizungumza mara baada ya makabidhiano ya nyumba iliyojengwa na Ttaasisi ya NOHA amesema Serikali kwa kushirikiana na Taasisi hiyo imeona ipo haja ya kufanya hivyo ili kumpunguzia usumbufu aliyokuwa akiupata hivyo amemuomba Mama huyo kuitumia Nyumba hiyo kwa malengo yaliokusudia ili kujenga uaminifu kwa Wafadhili hao kuendelea kuisaidia Jamii
Mkurugenzi wa Taasisi ya NOHA Mama Park amesema Taasisi yake itaendelea kustawisha maisha ya Jamii ya Wazanzibari wakiwemo wenye ulemavu na wenye hali ngumu za kimaisha ili kuyainua makundi hayo
Mkurugenzi Ustawi wa Jamii na Wazee Mwalim Hassan iIbrahim wameitaka Jamii hasa akina Baba kuacha tabia ya kuzitelekeza Familia zao pindi wanapopata Watoto wenye ulemavu kwani kufanya hivyo ni kuzikufuru neema za Mwenyezi Mungu
Mama mzazi wa Mtoto mwenye ulemavu Ndg.Siti Khamis Rashid ameipongeza Serikali na Taasisi ya NOHA kwa juhudi zao na kuahidi kuitumia msaada huo kwa malengo yaliokusudia .
Zaidi ya Shilingi Milioni 25 zimetumika kujenga Nyumba hiyo ikiwa ni msaada kutoka Taasisi ya NOHA