Serikali ya Mapinduzi ya zanzibar imetiliana Saini ya makubaliano na Ubalozi wa Sweeden ili kusaidia kuimarisha Sekta ya Elimu Nchini.
Akizungumza katika hafla ya utiaji Saini huo katibu Mkuu Ofisi ya Raisi Fedha na Mipango Dkt Juma Malik Akili amesema lengo la makubaliano hayo ni kuanzisha mradi utakaosaidia kukuza Sekta ya Elimu kwa kuwajengea uwezo wa kufundisha Watendaji pamoja na kuimarisha Miundo mbinu ya Madarasa.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na mafunzo ya amali Zanzibar Khamis Said amesema watahakikisha wanaimarisha Elimu ya awali na msingi kwa wanatumia Mtaala wa kisasa na mahiri pamoja na kuandika Vitabu mbali mbali ambayo watatumia Wanafunzi katika kujifunza.
Mwakilishi kutoka Nchini Sweeden Charlotta Ozaki Macias amefahamisha kuwa makubaliano hayo yamelenga kuisaidia Tanzania katika Sekta ya Elimu pamoja na kukuza Uchumi wa Nchi.