SMT NA SMZ ZIMEJIPANGA KUFANIKISHA MKUTANO WA WANACHAMA WA JUMUIA YA MADOLA

BALOZI DKT PINDI HAZARA CHANA

Wizara ya Katiba na Sheria ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zimejipanga vyema katika kufanikisha Mkutano wa Mawaziri wa Sheria wa Nchi Wanachama wa Jumuia ya Madola.

Akizungumza na Vyombo vya Habari Waziri wa Katiba na Sheria wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Balozi Dk Pindi Hazara Chana amesema lengo kuu  la Mkutano huo ni kujadili jinsi maendeleo ya Kidigitali yanavyowezesha upatikanaji wa haki kwa Watu hatua ambayo itaisaidia Tanzania kurahisisha ufanyajikazi katika masuala mbali mbali ya kisheria ikiwemo Mahakama na kuleta maendeleo katika Sekta hiyo. 

Waziri wa katiba Sheria utumishi na Utawala bora Mh. Haroun Ali Suleiman amesemea Mkutano huo ambao utafanyika kwa mara ya kwanza Zanzibar utaleta tija kubwa kwa Tanzania  katika nyanja mbalimbali ikiwemo Siasa, Uchumi na Utalii.

Mkutano huo unaotarajiwa kufanyika Tarehe Nne hadi Nane utafunguliwa na Raisi wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh Dk Samia Suluhu Hassan na kufungwa na Raisi wa Serikli ya Mapinduzi ya Zanzibar Dk Hussein Ali Mwinyi ambapo utawashirikisha Takribani Washiriki Miatatu kutoka Nchi 56 za jumuia ya Madola.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.