Mamlaka ya Kkudhibiti na Kupambana na Dawa za Kkulevya Tanzania DCEA imewataka Vijana wenye Umri wa Miaka 14 hadi 45, kujihadhari na matumizi ya Dawa za kulevya yanayoweza kuathiri Afya zao na kusababisha Taifa kupoteza nguvu kazi.
Ushauri huo umetolewa Mwanza na Afisa wa Mamlaka hiyo Kanda ya Ziwa Ndg.Dezidel Tumbu wakati akitoa Elimu kuhusu Madhara ya Dawa za Kulevya kwa Vijana wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Tanzania Saut na Chuo cha Afya City College Wilaya wa Magu.
Mdau wa mapambano dhidi ya Dawa za kulevya Ndg.Charles Waryoba amewataka Vijana kujisimamia na kutokubali kutumiwa kwenye biashara ya usafirishaji na utumiaji wa Dawa za Kulevya.
Nao Vijana wameahidi kuifikisha Elimu kuhusu madhara ya Dawa za kulevya waliyoipata kwa kuhakikisha Wanafunzi na Makundi mbalimbali ya Kijamii wanajiepusha na matumizi ya Dawa hizo.