MASHEIKH ,WANAZUONI , NA MAMUFTI AFRIKA WAOMBEWA DUA

dua

    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema ustawi wa maisha umechangiwa na kazi kubwa walioifanya Masheikh pamoja na Waalimu wa Dini waliotangulia mbele ya haki.

     Dkt.Mwinyi ameyasema hayo alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Dua ya kuwaombea Mufti, Masheikh, na Wanazuoni ambao walikuwa na mchango mkubwa Afrika na baadae kuiombea baraka na amani Tanzania na Afrika kwa ujumla dua iliyofanyika Viwanja vya Msikiti Mkuu wa Bakwata Jijini Dar es salaam pamoja na kusisitiza umuhimu wa umoja na mshikamano wa Taifa katika kudumisha amani na kuendeleza mafundisho ya uadilifu hasa kuanzia ngazi ya Familia na Jamii nzima.

    Aidha Dkt. Mwinyi ametoa shukrani kwa Bakwata kwa kuandaa dua hiyo ya kuwaombea Wanazuoni wa Afrika.

     Nae Mufti Mkuu wa Tanzania Alhaj Sheikh Aboubakar Bin Zubeir akatoa historia fupi kwa baadhi ya Wanazuoni waliokwisha kutangulia mbele ya haki akiwemo Sheikh Hassan Bin Ameir ambae anatokea Zanzibar.

Tags
stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.