WANAFUNZI GEITA WALIA NA HUDUMA YA VYOO

Geita Wanafunzi

    Zaidi ya Wanafunzi 1500, wa Shule ya Msingi Ludeba katika Kijiji cha Ludeba, Kata ya Ipalamasa, Wilaya ya Chato Geita wanakabiliwa na  ukosefu wa Vyoo vya kisasa hali inayosababisha  taaluma kushuka.
   Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhandisi Deusdedith Katwale amewashauri Wananchi wa Kata ya Ipalamasa  kuhakikisha anasimamia upatikanaji wa huduma muhimu katika Shule ya Msingi Ludeba na Serikali inaendelea kuimarisha miundo mbinu ya huduma za Kijamii.

    Deusdedith amebainisha hayo  wakati wa Ziara ya kutembelea Shule za Kata ya Ipalamasa kuona maendeleo ya Kijamii katika Wilaya hiyo.

    Mwalimu Mkuu wa Shule hio Ndg.Daudi William amesema kuwa Shule yake inakabiliwa na tatizo la Vyoo  na kusababisha   mahudhurio ya Wanafunzi kuwa mabaya..

    Afisa Elimu Wilaya ya Chato Ndg.Theobad Katama amewaomba Wananchi kushirikiano na kufanya utaratibu wa kusaidia kutatua tatizo hilo.

 



 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.