ORODHA YA WAPIGA KURA WAPYA KUWEKWA WAZI

ZEC

   Tume ya Uchaguzi Zanzibar imetangaza kuweka wazi Orodha ya Wapiga Kura Wapya katika Vituo vilivyotumika uandikishaji kwa Unguja na Pemba kwa muda wa Siku Saba.

    Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jaji George Joseph Kazi ameyasema hayo katika Ukumbi wa Sheikh Idris Abdulwakil Kikwajuni kwa Wadau wa Uchaguzi kuhusu uandukishaji wa Wapiga Kura Wapya na uwekaji wazi Orodha za Wapiga Kura .

    Amesema  utaratibu huo utaanza Tarehe Mosi Mwezi wa Tatu hadi Tarehe Saba kwa  lengo la  kutoa nafasi kwa Muombaji aliyeandikishwa kuwasilisha malalamiko ya kurekebisha Taarifa zao

    Akizungumzia Tathmini ya uandukishaji wa Wapiga Kura Wapya Awamu ya kwanza 2023 Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Ndg.Thabit Idarous Faina amesema Tume ya Uchaguzi Zanzibar kabla ya kuanza uandukishaji ilivishirikisha Vyama vya Siasa kwa kuwapa Mafunzo Mawakala wa Vyama vyao kwa utaratibu wa kuwemo katika Vituo vya uandukishaji. 

     Mkuu wa Kurugenzi ya Huduma za Uchaguzi Ndg. Khamis Issa Khamis amesema Taarifa ya  uwekaji wazi wa Orodha ya Wapiga Kura hadi kufikia 14 Mwaka 2024 Jumla ya Wapiga Kura Mia Tatu na Mbili wamewasilisha Maombi ya kuhamisha Taarifa zao kutoka Eneo moja na kwenda eneo jengine la Kupiga Kura 

    Tume ya Uchaguzi Zanzibar imeandikisha Wapiga Kura Wapya Awamu ya Kwanza katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kuanzia Tarehe 02 Disemba 2023 hadi Tarehe 15 Januari 2024 ikiwa ni Maaandalizi ya Uchaguzi  Mkuu kwa Mwaka 2025 ambapo Jumla ya Wapiga Kura Wapya Hamsini na Saba Elfu Mia Nane na Themanini  na Tatu Unguja na Pemba Wameandikishwa. 

 

 

 

 

 

 

 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.