MASHEHA KUSIMAMIA USAFI WA MAZINGIRA KATIKA MAENEO YAO

MH BAKAR MAGARAWA

Masheha wa Mkoa wa Mjini Magharibi wamesisitizwa kusimamia vyema usafi wa Mazingira katika maeneo yao ili kuondokana na mazalia ya Mbu wanaosababisha Malaria na Maradhi mengine.

Akifungua Mkutano kwa Masheha wa Mkoa wa Mjini Magharibi unaohusiana na hali ya Malaria Nchini Mkuu wa Kitengo cha Elimu ya Afya kutoka Wizara ya Afya Bakari Magarawa amesema kwa sasa Wilaya ya Mjini inaongoza kwa Malaria kutokana na kuwepo kwa sababu mbali mbali zikiwemo mabadiliko ya TabiaNchi pamoja na hali ya Mazingiza, hivyo amewataka viongozi hao wa Shehia kusimamia usafi ili kuondokana na Maradhi hayo. 

Akizungumzia suala la Macho Mekundu Magarawa amewataka Masheha hao kuwaelimisha Wananchi kutotumia Dawa zisizo Rasmi kutibu Macho na badala yake kufika katika Vituo vya Afya kupata Matibabu ya Maradhi hayo. 

Afisa Afya ya Jamii kutoka Wizara ya afya Programu ya kumaliza Malaria Zanzibar Mwinyi Khamis amesema imeripotiwa kuwa zaidi ya Wagonjwa Elfu tano wa Malaria Mwaka huu. 

Sheha wa Shehia ya malindi Hassan Masoud Ali na Sheha wa Shehia ya Sebleni Mohamed Mussa wamesema watahakikisha wanasimamia vyema suala la usafi wa Mazingira katika shehia zao ili kuondokana na mazalio ya Mbu.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.