BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU ZANZIBAR KUFANYA MAGEUZI SHERIA YA MIKOPO

MHE. LELA MOHAMED MUSSA

Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Zaznibar imekusudia kufanya mageuzi wa Sheria ya Mikopo kwa lengo la kutoa fursa kwa Wanafunzi wa Ngazi ya Stashahada kuweza kupata mikopo ya Elimu ya juu na kupata wanufaika wengi zaidi.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Mohamed Mussa ameyasema hayo huko Chukwani wakati wa Mafunzo ya Mswaada wa Sheria mpya ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi.

Amesema mabadiliko ya Sheria hiyo yamekuja kutokana na mwendelezo wa mabadiliko katika sekta ya Elimu kwani Serikali imeweka kipaumbele katika Ngazi ya Elimu ya ujuzi hivyo kuwa na Wanafunzi wengi wanufaika kwa Ngazi ya Stashahada kutawawezesha kupata fursa ya kusoma katika Ngazi ya Elimu ya juu. 

Akiwasilisha Mswada wa Sheria hiyo mpya ya Mikopo ya Elimu ya juu Zanzibar Mwanasheria wa Bodi hiyo Khamis Haji Omar amesema sheria hiyo imeweza kuipa uwezo Bodi ya Mikopo kufanya uwekezaji kwa lengo la kuiendeleza taasisi hiyo kwa maslahi ya Taifa. 

Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wamesema Kuna umuhimu kwa Bodi hiyo kuhakikisha inawanufaisha Wanafunzi wengi pamoja na kuangalia kwa kina Sheria zinazowekwa ili zisije kuleta athari wa Wanafunzi na Taifa kwa ujumla.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.