HUDUMA YA PATA DAWA NI MUHIMU KWA WATANZANIA

NAIBU WAZIRI WA AFYA

Wizara ya Afya Zanzibar imeitaka Kampuni ya Simu ya Mkononi Tigo Zantel na Laina Finance Limited kuhakikisha wanafuata misingi ya faida inayozingatia Ubinaadamu na sio kukomoa Wananchi katika huduma ya pata dawa.

Naibu Waziri wa Afya Mhe Hassan Khamis Hafidh, ameeleza hayo alipozindua huduma ya PATA DAWA kupitia Simu ya Mkononi Tigo Zantel kwa kushirikiana Laina Finance Limited huko Golden Tulip Uwanja wa Ndege.

Amesema huduma hiyo ni muhimu kwa maisha ya Watanzania kwani Wananchi wengi ni wangonge hivyo ni muhimu kuwasaidia katika mambo mbalimbali.

Mufti Mkuu wa Zanzibar Shekh Saleh Omar Kaabi, amesema mfumo huo ni miongoni mwa mambo muhimu anayohitaji Binaadamu hivyo kuwepo kwake kutawasaidia Wananchi kupata huduma za Afya za uhakika.

Mkurugenzi Tigo Zantel, Aziz Said Ali, na Afisa Mkuu wa Tigo Pesa Angelica Pesha wamesema Kampuni hiyo inatengeneza Historia kwani huduma ya Pata Dawa ni ya Kidijitali ambapo Tanzania ni Nchi ya kwanza kutoa huduma hiyo kwa Afrika Mashariki.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.