Afisa Mdhamini Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais Ndg.Ahmed Abuubakar Mohammed, amewataka Wamiliki wa Viwanda kuzingatia utunzaji wa mazingira na afya za Wafanyakazi ili kuepukana na athari zinazoweza kujitokeza.
Ametoa kauli hiyo huko Vitongoji Kisiwani Pemba katika Ziara ya kukagua Kiwanda cha Kokoto na Kiwanda cha kuhifadhi na kuchoma taka za Hospitali, Amesema Serikali kupitia Mamlaka ya usimamizi wa mazingira imeandaa
Miongozo maalumu kwa wawekezaji Nchini juu ya utunzaji wa mazingira na usalama wa Wafanyakazi hivyo Wawekezaji hao wanapaswa kufuata miongozo hiyo ili kuepuakana na madhara yanayoweza kujitokeza.
Aidha Afisa Mdhamini huyo amewataka Wakulima wa Mpunga katika Bonde la Kikoma, Kilimoni, Ziwani na Jaalani Mkoani ambao Mashamba yao yameathirika na maji ya Chumvi kutunza mazingira katika Mabonde hayo ikiwemo kutokukata Mikoko ili kuondoakana na changamoto inayowakabili.
Nao Wakulima hao wameahidi kuyafanyia kazi maelekezo hayo sambamba na kuiomba Serikali kuwapatia msaada wa dharura ili kukabiliana na athari zinazojitokeza.
Katika Ziara hiyo ya Siku Mbili Afisa Mdhamini huyo ametembelea kiwanda cha Maji cha Water Com kilichopo Kinyikani, Sheli ya Mafuta iliyopo mMzambarauni pamoja na Hoteli ya Mantarif iliyopo Makaangale pamoja na kuzungumza na Uongozi na Wafanyakazi wa Kampuni hizo.