Akizungumza Wakati Alipofungua Jengo La Huduma Za Tiba Za Dharura Na Maabara Huko Makunduchi Dkt Mwinyi Amesema, Katika Mwaka Wa Fedha 2023/2024 Serikali Imekusudia Kujenga Majengo Mapya Na Vifaa Tiba Vya Kisasa Ili Kuhakikisha Zinapatikana Kwa Wakati.
Amesema Kujengwa Kwa Jengo Hilo Itasaidia Kupatikana Kwa Wakati Huduma Za Afya Na Kupunguza Vifo.
Akitoa Maelezo Ya Kitaalamu Kaimu Katibu Mkuu Wa Wizara Ya Afya Zanzibar Dkt Amour Suleiman Mohamed, Amesema Lengo La Kujengwa Kwa Jengo Hili Ni Kuwapatia Matibabu Ya Dharura Na Uchunguzi Wa Wananchi Kwa Wakati.
Naibu Waziri Wa Afya Hassan Khamis Hafidh Amewataka Wahudumu Wa Afya Kutoa Huduma Bora Kwa Wananchi.
Nao Wafadhili Wa Mradi Wa Kuimarisha Afya Zanzibar Simon Kuhnert Na Mukhtar Karim Kutoka The Lady Fatemah Chartable, Wameahidi Kuendelea Kushirikiana Na Serikali Ili Kuimarisha Afya Za Wazanzibari.
Jengo Hilo La Huduma Za Dharura Na Tiba Za Maabara Katika Kituo Cha Afya Makunduchi Limegharimu Shilingi Milioni Mia Sita Na Hamsini.