Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said amesema hayo katika Mkutano wa kutathmini utendaji na kupanga mikakati ya ukusanya Kodi kwa nusu ya pili kwa Mwaka 2023/2024 huko Hotel ya Madinatul Bahar Mbweni Mjini Unguja.
Amesema usimamizi mzuri kwa Watendaji kunasaidia kuleta ufanisi katika kazi na kuimarika kwa mifumo ya ukusanyaji wa Mapato kunaharakisha maendeleo ya Taifa.
Akizungumza katika Mkutano huo Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya mapato Zanzibar ZRA Yussuf Juma Mwenda amesema ufanisi wa ukusanyaji wa kodi kwa nusu ya kwanza ya Mwaka umeongezeka na lenga kuwa nusu ya pili ya Mwaka hali hiyo iongezeke mara dufu.
Akiwasilisha Njia za kupata taarifa za Wageni wanaoingia Nchini Mkurugenzi mfumo wa kukusanya kodi Mtandaoni Masoud Moh'd Mbarouk amesema kuna tatizo ndogo katika ukusanyaji kupitia Mtandao huo ila bado wanaendelea kutafuta njia ya kuondoa tatizo hilo.
Mwenyekiti wa bodi ya zra Prof. Hamed Rashid Hikman amewataka Wafanyakazi kuwa Waadilifu na Waaminifu kwa walipakodi ili waendelee kulipa kodi kwa hiari.