Akitoa Shukurani Kwa Taasisi Ya Majlis Al-Maarif Mara Baada Ya Kupokea Vifaaa Vya Kushajihisha Uchangiaji Damu, Mkurugenzi Huyo Amesema Mahitaji Ya Damu Yameongezeka Kulingana Na Ongezeko La Majengo Ya Hospitali Hivyo Kuna Umuhimu Wa Kuchangia Damu.
Mwenyekiti Wa Taasisi Ya Majlis Almaarif Tahir Khatib Tahir Amezitaka Taasisi Za Dini, Chama Na Serikali Kujitokeza Kuchangia Damu Ili Kuhakikisha Wanaohitaji Waweze Kupata Huduma Hiyo Kwa Uhakika.
Afisa Uhusiano Na Masoko Taasisi Ya Mpango Wa Damu Salama Ussi Bakar Mohammed Amesema Msaada Huo Utaongeza Nguvu Ili Kupata Damu Ya Kutosha.
Benki Ya Damu Salama Imepokea Msaada Wa Vitu Mbali Mbali Ikiwemo Vyakula Na Vinywaji Katika Kusherehekea Miaka 60 Ya Mapinduzi Ya Zanzibar.
stories
standard