SERIKALI IMESEMA INA NIA YA KULIBADILISHA ENEO LA DIMANI KUWA LA KIBIASHARA LA KIMATAIFA.

MAONESHO

Akifungua Maonesho Ya 10 Ya Biashara Ya Kimataifa, Rais Wa Zanzibar Na Mwenyekiti Wa Baraza La Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi Ikiwa Ni Mwendelezo Wa Shamrashamra Za Miaka 60 Ya Mapinduzi Ya Zanzibar Dk Mwinyi Amesema Serikali Imekusudia Kujenga Majengo Mbali Mbali Ya Kisasa Ya Biashara Na Kwa Sasa Wameanza Na Eneo La Nyamanzi Wilaya Ya Magaharbi B, Ambapo Tayari Kashakabidhiwa Mfano Wa Ramani Ya Mji Mpya Wa Biashara Na Uwekezaji Wa Eneo Hilo Waziri Wa Biashara Na Maendeleo Ya Viwanda Wa Zanzibar.

Amesema Mpango Huo Utatoa Fursa Ya Kukuza Biashara Na Uwekezaji Na Kuitangaza Zanzibar Kimataifa.

Dk. Mwinyi Amezitaka Taasisi Za Umma Na Binafsi Kulitumia Eneo Hilo La Biashara Kwa Shughuli Zao Mbalimbali Ili Kuendelea Kulitangaza Kiuchumi Ndani Na Nje Ya Nchi, Pamoja Na Kuwataka Wajasiriamali Wadogo Na Wakubwa, Wafanyabiashara Na Wadau Wengine Kuzalisha Bidhaa Zenye Ubora Ili Kuendana Na Hadhi Ya Kimataifa.

Waziri Wa Biashara Na Maendeleo Ya Viwanda, Mhe Omar Said Shaaban Amesema Eneo Hilo La Biashara La Kimataifa Ni Fursa Ya Kukuza Na Kuendeleza Biashara Na Uwekezaji Nchini Hivyo Kuwekwa Kwa Maonesho Hayo Kutakuza Maendeleo Ya Nchi.

Katibu Mkuu Wizara Ya Biashara Na Maendeleo Ya Viwanda, Ali Khamis Juma Amesema, Ujenzi Wa Eneo Hilo La Biashara Umeanza Mwaka Jana Na Umegharimu Shilingi Bilioni 8 Nukta 2 Ambapo Umejumuisha Ujenzi Wa Miundombinu Ya Barabara Zote Za Eneo Hilo Ikiwemo Sehemu Za Maegesho Ya Magari, Maji Safi, Umeme, Na Mawasiliano, Na Uwekaji Wa Vigae Kuzuia Athari Za Mvua Na Tope Na Mitaro Ya Maji Machafu.

Maonesho Hayo Ya Kimataifa Yenye Kaulimbiu “Biashara Mtandao Kwa Maendeleo Ya Biashara Na Uwekezaji” Yamepewa Jina La “Zanzibar Internationa Trade Fair” Yanajumisha Wafanyabiashara Zaidi Ya 4,000 Kutoka Ndani Na Nje Ya Tanzania Ikiwemo Zambia, Burundi, Misri Na Uganda Yanajumuisha Wafanyabiashara Wakubwa, Wadogo, Taasisi Za Umma Na Binafsi, Kampuni Mbalimbali Pamoja Na  Wajasiriamali

 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.