NI FARAJA KUBWA KUONA WAZANZIBARI WANAJIVUNIA MATUNDA YA MAPINDUZI NA HUDUMA BORA

Mhe. Kassim Majaliwa

Waziri Mkuu Wa Jamuhuri Ya Muungano Wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Ameipongeza Wizara Ya Afya Kwa Kuweza Kutekeleza Sera Ya Afya Na  Kusimamia Vyema Miradi Ya Wizara Ya Afya.

 

Akifungua Hospitali Ya Wilaya Kaskazini B Pangatupu Ikiwa Ni Shamrashamra Za Miaka 60 Ya Mapinduzi  Ya Zanzibar Amesema Ni Faraja Kubwa Kuona Wazanzibari Wanajivunia Matunda Ya Mapinduzi Na Huduma Bora Za Kibingwa Zinapatikana 

Amefahamisha Kuwa Serikali Tayari Imejenga Hospital 10 Za Wilaya  Kwa Lengo La Kupunguza Msongamano Wa Wagonjwa Kwenye Hospitali Nyengine.

 

Waziri Wa Afya Mhe. Nassor Ahmed Mazrui Amesema Vituo Vya Afya 18 Vya Wilaya Ya Kaskazini B Vitaweza Kupeleka Rufaa Katika Hospital Ya Wilaya Pangatupu Na Katika Kuimarisha Huduma Za Afya Wizara Imepiga Hatua Kubwa Katika Kuondosha Tatizo La Matibabu Katika Vituo Vya Afya Vya Wilaya Na Mikoa.

 

Akitoa Taarifa Ya Kitaalamu Ya Wizara Ya Afya Kaimu Katibu Mkuu   Wizara Ya Afya Dr. Amour Moh'd Suleiman Amesema Hospital Ya Wilaya Pangatupu Imejengwa Kwa Fedha Za Uviko 19 Na Inauwezo Wa Kulaza Wagonjwa Miamoja Kwa Wakati Mmoja Pamoja Na Huduma Zote Muhimu .

 

Mkuu Wa Mkoa Wa Kaskazini Unguja Rashid Hadid Rashid Amesema    Serikali  Imetekeleza Miradi Mikubwa Ya Maendeleo Kupitia Sekta Za Elimu, Afya Na Masoko  Hivyo Ni Vyema Wananchi Kuthamini Juhudi Hizo  Kuitunza Miradi Hiyo Ili Iwe Endelevu 

Ujenzi Wa Hospital Ya Wilaya Pangatupu Hadi Kukamilika Kwake Umegharimu Shilingi Bilioni 8.9

 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.