SERIKALI INA KILA SABABU YA KUFANYA MABADILIKO KATIKA SEKTA YA BAHARINI ILI KUWEKA MAZINGIRA MAZURI YA USAFIRI WA BAHARI

rais mwinyi

Ameyaeleza hayo Rais Wa Zanzibar Dkt. Mwinyi Ambae Ameshuhudia Utiaji Saini Mkataba Wa Ujenzi Wa Bandari Ya Maruhubi Ikulu Zanzibar, Amesema Serikali Imeamua Kujenga Bandari Ya Maruhubi Kutokana Na Bandari Ya Malindi Kuzidiwa Na Abiria Pamoja Na Mizigo Na Kusababisha Msongamano.

Amesema Mradi Huo Utakuwa Mfano Mkubwa Wa Ushirikiano Wa Sera Ya Serikali Na Sekta Binafsi Ya PPP Katika Kufikia Malengo Ya Utekelezaji Wa Miradi Mbalimbali Nchini.

Waziri Wa Ujenzi Mawasiliano Na Uchukuzi Dkt.Khalid Salum Mohammed Amesema Mradi Huo Unatafsiri Maono Ya Dkt. Mwinyi Katika Vipaumbele Muhimu Vitakavyowezesha Ukuaji Wa Uchumi.

Akitoa Taarifa Ya Kitaalam Mkurugenzi Mkuu Wa Shirika La Bandari Akif Mohammed Amesema Katika Mradi Huo Ambao Utagharimu Dola Milioni 400 Utakaotekelezwa Kwa Miezi 36 Utakapokamilika Utahudumia Abiria Elfu Tano Kwa Wakati Mmoja.

Akitoa Salamu Za Kampuni Ya ZF Devco Itakayojenga Bandari Hiyo, Mkurugenzi Wa Kampuni Hiyo Ameipongeza Serikali Kwa Hatua Inazochukuwa Katika Uendelezaji Miradi.

 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.