SERIKALI ITAENDELEA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA MAWAKILI
Rais Wa Zanzibar Na Mwenyekiti Wa Baraza La Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Amekihakikishia Chama Cha Mawakili Zanzibar Kuwa Serikali Inathamini Na Kuunga Mkono Kazi Nzuri Inayofanywa Na Chama Hicho Ya Kuwasaidia Wananchi Katika Masuala Ya Kisheria.
Rais Dkt. Mwinyi Ameyasema Hayo Alipokutana Na Uongozi Wa Chama Cha Mawakili Zanzibar Ulioongozwa Na Rais Wa Chama Hicho, Wakili Joseph Shaban Magazi, Waliofika Ikulu, Zanzibar.
