WAZIRI WA BIASHARA AAHIDI KUTOA MASHIRIKIANO KWA BARAZA LA UDHIBITI MFUMO WA UTOAJI LESENI

Waziri wa Biashara

    Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Mhe.Omar Said Shaaban ameahidi kutoa ushirikiano kwa Baraza la Udhibiti Mfumo wa Utowaji wa Leseni ili kufikia malengo ya kuweka mazingira mazuri ya kibiashara nchini.

    Ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Bodi Mpya ya Baraza la Udhibiti Mfumo wa Utowaji wa Leseni katika ukumbi wa Ofisi za Baraza huku Malindi, Wilaya ya Mjini.

     Aidha amesema kazi kubwa ya baraza hilo ni kuhakikisha kuepuka uholela kwenye taasisi za Serikali kwa kazi zote zinazotoa leseni, ruhusa, vibali vya biashara zinaendeshwa kisheria.

     Alifafanua kuwa imani yake ni kuyasimamia na kuliendeleza vyema Baraza hilo kwa kufanya kazi kwa mashirikiano kwa kuendeleza viwanda nchini.

     Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi Ndugu Mohamed Aboud Mohamed amesema lengo la kuundwa Bodi hiyo ni kudhibiti uholela wa utoaji wa vibali, leseni na ruhusa ambazo husababisha gharama katika uendeshaji wa biashara.

     Hivyo Bodi inaendelea kutafuta mfumo mzuri utakaowezesha kufanyika kwa biashara vizuri zenye unafuu bila gharama kubwa ili kuifanya Zanzibar kuwa kituo kikubwa cha biashara katika ukanda wa Afrika Mashariki.

     Nae, Katibu Mtendaji wa Baraza la Udhibiti Mfumo wa Utoaji wa Leseni Ndugu Hawwah Ibrahim Mbaye amesema kwenye Baraza hilo mafanikio mengi yamepatikana katika kuongezea mapato kwa Serikali kupitia ukusanyaji wa kodi kwa njia ya kidigitali.

     Baraza linasimamia Mamlaka za Serikali 54 zinazosimamia utoaji wa vibali, leseni na vibali vya ufanyaji biashara, alisema Katibu Mtendaji Hawwah.

 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.