WAZIRI TABIA ATANGAZA KUREJESHA KAMATI YA SAZI

WAZIRI TABIA AKITOA TAARIFA

     Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo imetangaza kurejesha tena Kamati ya Saidia Zanzibar Ishinde (SAZI) ili kuisaidia Serikali kutafuta Fedha za kuziendesha Timu za Taifa Zanzibar.

      Akitoa Taarifa kwa Vyombo vya Habari huko Ofisini kwake Migombani Waziri wa Habari Utamaduni Vijana na Michezo Mhe.Tabia Maulid Mwita amesema hatua hiyo ni muhimu katika kujenga mazingira ya Ushindi na Hamasa kwa Michezo hapa Zanzibar.

    Aidha Waziri Tabia amezitaka Timu za Zanzibar zitakazoshiriki katika Mashindano ya Chalenji na Senior Cup kufanya jitihada za kutosha kwa lengo la kupata ushindi na kuitangaza Zanzibar Kitaifa na Kimataifa.

       Katika Hafla hiyo Waziri Tabia ameteuwa Wajumbe Kumi pamoja na kutja majukumu yao ili kuanza kazi haraka huku akisisitiza nidhamu Mashirikiano ili kufikia malengo.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.