Chama Cha Mapinduzi CCM kimesema hakitasusia maridhiano na Vyama vya Upinzani Nchini kwenye jambo lolote la kujenga na lenye Maslahi kwa Taifa na Wananchi wake.
Hayo yamebainishwa Jijini Dodoma na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Dkt.Emmanuel Nchimbi wakati akizungumza na Wanachama alipowasili kwa mara ya kwanza Makao Makuu Dodoma Tangu kuteuliwa.
Aidha Dkt.Nchimbi,amewataka wana CCM kuendelea kukilinda Chama na mshikamano uliopo kwa sasa.
Wakati huo huo Dkt.Nchimbi amewapokea Wanachama wapya ambao wamewahi kushika nafasi mbalimbali ndani ya Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema.
stories
standard