WAJUMBE WASHAURI FEDHA ZA BAJETI YA SERIKALI KUANGALIA MIUNDOMBINU .

BARAZA LA WAWAKILISHI

 

Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi  wameishauri  Fedha.   Za  Bajeti ya Serikali kuangalia  Vipaumbele vya  Ujenzi wa Miundombinu  ya Barabara ,Maji pamoja na Uimarishaji  wa uendelezaji wa Viwanja. Vya Ndege.

  wamesema  ili mambo hayo yaweze kufanikiwa  Wajumbe hao wameishuri Serikali   kuingiza Fedha za Bajeti  kwa Wakati ili ziweze kuharakisha  maendeleo  ya haraka hasa katika upatikanaji wa huduma ya Maji la muda mrefu.

Wajumbe hao wametoa michango hiyo wakati wakijadili mpango wa Maendeleo ya wa Serikali  kwa Mwaka wa Fedha 2024/ 2025  katika Kikao cha Bajeti cha Baraza la Wawakilishi kinachoendelea Chukwani.

Wameisisitiza Serikali kuharakisha  kuelekeza nguvu zake katika suala la uchimbaji  wa Mafuta na Gesi   kwa kuwa na Bajeti ya Fedha za kutosha kuhakikisha  Nishati hyo   inafanikiwa.

Wakichangia Sekta ya uwekezaji Wajumbe hao  wamesema bado kuna Visiwa  ambavyo ni Vivutio vya Utalii  walivopewa wawekezaji  ambavyo hadi sasa havija  endelezwa hivyo  vinahitaji kuangaliwa upya na Serikali  kwa kuvifanyia maamuzi

Wameishauri   Serikali kuboresha Mifumo ya Fedha ya ndani  ili kupunguza upotevu wa Fedha    pamoja na kupunguza misamaha ya Fedha za Kodi kwa Wafanyabiashara.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.