WAFANYAKAZI KUZINGATIA SHERIA ZA KAZI

MHE. ALI SULEIMAN AMEIR

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Zanzibar, Mhe Ali Suleiman Ameir amewataka Watendaji wa Ofisi hiyo kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Miongozo ili kufikia malengo na matarajio ya Serikali.

Akizungumza na Wakuu wa vitengo wa Ofisi ya Rais Ikulu wakati wa kujitambulisha mara baada ya kuteuliwa hivi karibuni amesema ni vyema kwa Watendaji kutekeleza Majukumu yao ya Msingi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Miongozo ili kufikia maendeleo endelevu.

 katika hatua nyingine Waziri huyo amewaagiza Watendaji hao kuhakikisha wanapitia upya Sheria na kanuni zilizopitwa na wakati ambazo haziendani na kasi ya Serikali ya awamu ya nane.

Viongozi wa vitengo hivyo wamewasilisha Mafanikio, na matatizo katika Vitengo vyao huku wakisisitiza umoja na mshikamano katika utekelezaji wa Majukumu yao.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.