Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan, amewataka Viongozi wa Chama hasa wa Matawi kuwashawishi Vijana kujiunga na CCM ili kiweze kupata Wanachama wengi na kukiwezesha kushinda katika uchaguzi wa Mwaka 2025.
Dk. Samia alieleza hayo wakati akizindua Tawi kisasa la CCM Tasani Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja ikiwa ni muendelezo wa ziara yake katika Mikoa ya Kichama amesema anaamini bado Vijana wengi hawajajiandikisha hivyo ni vyema kuwashawishi ili kuendelea kukipa nguvu Chama chao kiendelee kuchukua ushindi
Rais Samia amesema Uanachama na Uimara wa Chama cha CCM ni Wanachama wenyewe kuwa imara, kuwa wamoja na kujitambua kuwa wao ni wafuasi wa chama hicho.
Dk.Samia amesema ni lazima kuhakikisha Matawi ya Chama yanafanya Kazi kwa njia ya kisasa za kutunza kumbukumbu za Wanachama kwa njia ya Kielektroniki hatua ambayo itawezesha kujua idadi ya wanachama wao.
Hata hivyo, amesema imani yake Viongozi wa chama waeendelee kuimarisha Matawi mengine ya Chama ili Wanachama kuvutiwa zaidi.
Akizungumzia uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba Mwaka 2025, Rais Samia aliwaaasa Viongozi kuacha kuhujumiana na kuhakikisha wale wanaotenda kazi basi kupatiwa nafasi.
Akisoma Risala ya Tawi hilo,amesema Tawi la Tasani Makunduchi Ndugu Abeid Kitwana Haji amesema wameunda Darasa la itikadi lenye Wanafunzi 168 wakiwemo 56 Wanaumme na Wanawake 112 na ifikapo Mwezi Febuari mwaka 2024 Darasa hilo litamaliza mafunzo hayo na wote kupatiwa Kadi za Uanachama na jumuiya zake ili kuongeza idadi ya Wanachama katika Tawi hilo iliwatajitokeza kupiga kura na kukiwezesha Chama kupata ushindi.
Mbunge wa Jimbo la Makunduchi Mh Rafii Idarusi Faina ametoa shukrani kwa Mwenyekiti wa CCM nakuahidi kutekeleza kwa vitendo ahadi walizoziahidi kwa Wananchi.
Katika ziara hiyo pia Rais Samia amesalimiana na kuzungumza na Wananchi na wanaCCM wa Tawi la CCM Kitogani na Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja.