Naibu Waziri wa maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe Anna Athanas Paul amewasisitiza Vijana na Wanafunzi Kutojirikodi na kujirusha katika Mitandao ya Kijamii ili kujiepusha na Matatizo yatakayo jitokeza.
Akizungumza katika Madhimisho ya Siku ya Familia Duniani Naibu Waziri huyo amesema ili kulinda Maadili na Malezi bora kwa Watoto ni vyema kwa Wazazi kuwasimamia Watoto pamoja na kuwasisitiza Vijana kuacha Tabia za kujituma katika Mitandao ya Kijamii na badala yake kuitumia kwa kuwaletea Faida.
Wakiwasilisha mada ya Malezi Bora na Afya ya Akili Daktari wa Magonjwa na Afya ya Akili Makame Haji Pandu na Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Watoto Mohamed Jabir wamesema ni vyema kwa Wazazi kuwalea Watoto kwa kufata Mila ,Silka na utamaduni ili kumjenga Mtoto katika misingi bora.
Mwenyekiti wa Elimu ya Watu Wazima Zanzibar Abubakar Ali Suleiman amesema lengo la kuandaa Mafunzo hayo ni kuadhimisha Siku ya Familia Duniani kwa kutoa Elimu pamoja mbinu za kuimarisha Familia zetu ili kuitunza Jamii katika maadili mema.
Washiriki waliyopatiwa mafunzo hayo wamesema wamefarajika kwa kupatiwa Mafunzo hayo ambayo yatawasaidia kujua namna gani wanaishi na Familia zao kwa ushirikiano mzuri.