TFF YAANZA MIKAKATI YA KUIBUA VIPAJI

Michezo mashuleni

   Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeanza mkakati wa kuibua Vipaji vya Mpira wa Miguu kwa kuzipatia Mipira Mia Mbili Arobaini Shule za Msingi Sita za Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro 

    Akikabidhi Mipira hiyo kwa Walimu wa Shule hizo za Msingi Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Morogoro (MRFA) Paschal Kihanga amesema lengo la TFF na Serikali ni kuhakikisha wanatengeneza Vipaji vya Mpira kuanzia Watoto Wadogo.

  Katibu Tawala Wilaya ya Kilosa Salome Mkinga amewataka Walimu wa Michezo kwenye Skuli za Msingi Wasimamie Michezo ipasavyo ili lengo lililokusudiwa lifanikiwe.

    Afisa Michezo Wilaya ya Kilosa Paula Katololo ameelekeza kuwepo kwa usawa wa utumiaji wa Mipira hiyo baina ya Watoto wa Kiume na wa Kike ili kukuza Vipaji vya  Michezo.

Tags
stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.