WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ATAKA MAZINGIRA WEZESHI KWA VYOMBO VYA HABARI.
Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa, amezitaka Mamlaka zinazosimamia Sekta ya Habari Nchini, kuimarisha Mazingira wezeshi kwa Waandishi wa Habari za Mitandaoni, ili kufikia uchumi wa Kidijitali.
akizungumza katika Kongamano la Wamiliki wa Vyombo vya Habari za Mtandaoni, Mhe Kassim amesema Serikali itaendelea kushirikiana na Wadau wa habari za Mitandao ya Kijamii na Vyombo vya Habari, ili kuharakisha ukuaji wa maendeleo Nchini.